Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 06:10

Kenya yakubali kufungua kambi nyingine ya Wakimbizi


Wakimbizi wakiwa katika msitari kupata msaada
Wakimbizi wakiwa katika msitari kupata msaada

Kambi hiyo itafunguliwa baada ya mvutano wa siku kadha baina ya makundi ya misaada na idara za serikali ya Kenya

Kenya imekubali kufungua kambi mpya ya wakimbizi karibu na mpaka wake ulio karibu na Somali huku maelfu ya watu wakitoroka ukame ambao umekumba Somalia. Waziri Mkuu nchini Kenya Raila Odinga alisema kuwa kambi ya Ifo II ambayo inaweza kuwa na watu 80,000 itafunguliwa kwa siku kumi zajazo.

Zaidi ya watu milioni 11 wanahitaji msaada wa dharura kutokana na njaa. Bw. Odinga alisema kuwa ijapokuwa taifa la Kenya linakabiliwa na tisho la usalama, hawawezi kuwakufukuza wakimbizi. Alikosoa wtau wanaosema kuwa awali Kenya ilikuwa imekataa kufungua kambi ya Ifo II.

Kenya imekuwa na wakimbizi kwa muda wa miaka 20 na imekuwa ikiomba usaidizi kutoka jamii ya kimataifa. Hata hivyo waziri mkuu alisema Kenya haitachukuwa jukumu la kuwgharamia wakimbizi hao.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kamishna mkuu wa shirika la umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi –UNHCR Antonio Guterres kuzuru Somali pamoja na kambi hiyo ya Daadab na kusema kuwa hali hiyo ni janga kubwa la kibinadamu ulimwenguni.

XS
SM
MD
LG