Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 12:06

Kenya yaimarisha ulinzi kaunti ya Marsabit kufuatia ghasia za kikabila

Wafugaji katika kaunti ya Marsabit nchini Kenya wakipeleka wanyama kunywa maji. (Picha na Reuters).
Wafugaji katika kaunti ya Marsabit nchini Kenya wakipeleka wanyama kunywa maji. (Picha na Reuters).

Kenya imepeleka maelfu ya polisi na maafisa wengine wa usalama katika eneo lenye hali tete la kaunti ya Marsabit kufuatia kuzuka kwa ghasia za kikabila.

Kenya imepeleka maelfu ya polisi na maafisa wengine wa usalama katika eneo lenye hali tete la kaunti ya Marsabit kufuatia kuzuka kwa ghasia za kikabila.

Serikali inasema ukame, uchochezi wa kisiasa na kuwepo silaha kutoka nchi jirani ya Ethiopia vinastahili kulaumiwa kwa kudorora kwa hali ya usalama kwenye eneo la mpakani.

Amri ya kutotoka nje wakati wa usiku imewekwa kwa mwezi ujao na zoezi la kusalimisha silaha linatarajiwa kuanza.

Wizi wa ng’ombe umeongezeka sana huko Marsabit ambayo ni moja ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na ukame kote katika Pembe ya Afrika.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya amesema polisi wamekamata idadi kubwa ya silaha na risasi zilizoingizwa kimagendo kutoka kusini mwa Ethiopia ambako vikosi vya serikali vinapambana na waasi kutoka jeshi la ukombozi la Oromo.

XS
SM
MD
LG