Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 02:46

Kenya yaadhimisha Madaraka Day


Kundi la wanamgambo wa al-Shabab la nchini Somalia latoa kitisho cha kushambulia majengo marefu mjini Nairobi

Kundi la al-Shabab latoa kitisho cha kufanya mashambulizi mengine kwenye majengo makubwa mjini Nairobi wakati Kenya ikisheherekea Madaraka Day

Kenya imeadhimisha June mosi miaka 49 tangu kujipatia uhuru wa ndani kutoka koloni la Uingereza. Sherehe rasmi zilifanyika mjini Nairobi na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali pamoja na Rais Mwai Kibaki ambaye alilihutubia taifa.

Rais Kibaki aliwaambia wakazi wa Kenya kwamba malumbano ya kisiasa yanayoendelea nchini humo yanatoka kwa wanasiasa wenyewe nchini humo.

Aliwahakikishia wananchi kwamba utaratibu wa kukabidhi madaraka utawala mpya baada ya uchaguzi mkuu ujao utafanyika kwa amani na utulivu.


Wakati huo huo kundi la wanamgambo wa ki-Islam la Al-Shabab limetoa kitisho kwamba litashambulia majengo merefu yaliopo mjini Nairobi katika muda wa wiki mbili zijazo.

Tangu serikali ya Kenya ilipoamua kupeleka wanajeshi wake nchini Somalia kupambana na wanamgambo wa Al-Shabab nchi hiyo imekuwa ikipata mashambulizi mara kwa mara yanayosababisha vifo na watu kujeruhiwa.

Wakati huo huo kufuatia vitisho vya Al-Shabaab, wananchi nchini humo wameanza mtindo wa kuepuka mikutano ya hadhara, au makundi ya watu kufurika katika kumbi za starehe.

Mjini Mombasa na ukanda wa Pwani watu wengi wamesusia maeneo ya burudani, au kwenda kubarizi katika fuo za bahari.

XS
SM
MD
LG