Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 21:40

Kenya: Wanaharakati wavitaka vitengo vya serikali kumaliza  ukatili wa jinsia


Rais wa Kenya William Ruto
Rais wa Kenya William Ruto

Dunia ikiadhimisha siku 16 za uanaharakati, mashirika ya asasi za kijamii Kenya yameungana na wengine duniani kupinga ukatili wa kijinsia na mauaji ya wanawake ambayo yameshamiri na kuzua hofu miongoni mwa wanawake kenya.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:06 0:00

Mashirika ya asasi za kijamii na wanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto wa kike dhidi ya dhulma za kijinsia, wamehimiza serikali kuweka juhudi za pamoja na za dharura kukomesha ukatili wa kijinsia.

Ingawa Kenya imepiga hatua kwa kubuni sheria za kulinda haki za wanawake, utekelezaji ni dhaifu, huku ripoti za mauaji ya wanawake zikiongoza miongoni mwa dhulma zinazotekelezewa wanawake nchini.

Uanaharakati Dhidi ya Dhulma za Kijinsia

Wakizungumza pembezoni mwa maadhimisho ya uzinduzi wa siku 16 za uanaharakati dhidi ya dhulma za kijinsia, wanaharakati hao wamesema wakati umefika kwa vitengo vya serikali kuchukua hatua kumaliza ukatili wa jinsia.

Maureen Magak na Doris Ojiambo ni wanaharakati kutoka mashirka ya Lend A voice Africa na lile la collaboration for women in network, CWID.

Mbali na mauaji wanawake bado wanakabiliw ana dhulma nyenginezo ikiwemo dhulma za kinyumbani, kunyimwa haki za kurithi, nyingi zikisababishwa na ukosefu wa ufahamu kuhusu haki zao.

Africa Muslim Women Action Network

Shirika la Africa Muslim women action network, ambalo linapigania haki za wanawake waliolewa katika mahakama ndoa; changamoto kubwa ya kutoenea kwa hamasa kuhusu haki za wanawake ili kuzuia mauaji ni fedha.

Zuhura Hussein Mali, ni afisa wa mradi katika shirika hilo la AMWAN.

Vyombo vya habari, mikutano ya hadhara na vikao vya mazungumzo ni baadhi ya mbinu ambazo mashirika ya kutetea haki za binadamu wametumia kufikia jamii kuhusu haki zao.

Wanaharakati nchini Kenya wakiadhimisha siku ya Kimataifa ya Kuutokomeza umaskini huko Nairobi, tarehe 17 Januari 2020. Picha na TONY KARUMBA / AFP
Wanaharakati nchini Kenya wakiadhimisha siku ya Kimataifa ya Kuutokomeza umaskini huko Nairobi, tarehe 17 Januari 2020. Picha na TONY KARUMBA / AFP

Licha ya juhudi hizo bado visa vinaripotiwa, Coolins Mangicho , Naibu mwenyekiti wa klabu ya little theatre Mombasa kwa miaka 6 wanatumia Sanaa kupitisha ujumbe kwa kuhusisha watoto na vijana.

Uhaba wa fedha ukiwa na changamoto katika kufikia azima hiyo.

Haya yanajiri siku chache baada ya rais William Ruto kutangaza kuwa serikali imetenga shilingi milioni 100 kukabiliana na mauaj ya wanawake, fedha ambazo wanaharakati wanasema hawajahusishwa na hawana habari vipi zitatumika kumaliza kadhia hio.

Imetayarishwa na Amina Chombo wa VOA, Mombasa, Kenya.

Forum

XS
SM
MD
LG