Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 03:18

Uhuru kukutana na waziri wa Marekani Jumanne


Waziri wa mambo ya ndani wa Marekani Sally Jewell

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya anatazamiwa kufanya mazungumzo Jumanne na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani Sally Jewell mjini Nairobi kuhusu hifadhi ya wanyama pori.

Msemaji wa rais Manoah Esipisu alisema mkutano huo ni ufuatiliaji wa ahadi ya Rais Barack Obama kuhusu hifadhi ya wanyama pori barani Afrika. Moja ya swala la majadiliano katika mkutano huo itakuwa mikakati ambayo Kenya imetumia katika hifadhi ya wanyama.

Ripoti za hivi karibuni zilisema Kenya imepiga hatua kubwa katika kupambana na ujangili ambao umepungua kwa asilimia 80.

Waziri Jewell wa Marekani ambaye yuko katika ziara ya Kenya pia atatembelea maeneo mengine ya Kenya pamoja na ujumbe wake, ikiwa ni pamoja na mji wa Mombasa ambao sasa unapambana kurudisha biashara ya kitalii ambayo ilianguka kwa muda mrefu kutokana na sababu za kiusalama.

XS
SM
MD
LG