Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 07:31

Serikali kuboresha huduma za watalii Pwani ya Kenya


Mtalii akifanya mazoezi katika ufukwe wa pwani ya Mombasa, Kenya.
Mtalii akifanya mazoezi katika ufukwe wa pwani ya Mombasa, Kenya.

Serikali za kaunti katika maeneo ya utalii kwenye maeneo ya pwani nchini Kenya zimeanzisha hatua mahsusi kuongeza huduma katika maeneo ya watalii ili kuvutia watalii zaidi.

Ripoti kuhusu utalii Mombasa
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:12 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kulingana na maafisa wa kaunti pamoja wamiliki wa mahoteli ya kitalii juhudi za mafunzo sasa zinaendeshwa kwa wahudumu wa aina mbali mbali ili kuongeza ufanisi na kuvutia watalii zaidi.

Wadau katika sekta ya utalii wanasema kutokana na kutokuwa na usimamizi mzuri kuna wafanyabiashara mbali mbali ambao wanajaribu kutoa huduma kwa watalii lakini bila na mafunzo,a na matokeo yake ni kuwa na shughuli ambazo zinabughudhi watalii badala ya kuwavutia.

Sasa maafisa wa kaunti pamoja na wamiiliki wa mahoteli wanatoa mafunzo kwa wachuuzi wadogo wadogo ili kuboresha aina ya huduma ambazo zinapatikana katika maeneo ya watalii.

XS
SM
MD
LG