kufuatia hatua ya Kenya kuwapeleka nchini China kwa lazima raia watano wa Taiwan Jumatatu Balozi wa Nchi hiyo John Chen ameikosoa Kenya kuwatuma raia wake Beijing badala ya Taipei, Sasa Serikali ya Kenya imejitenga mbali na matamshi ya balozi huyo aliye na makao yake nchini Afrika Kusini.
Raia hao watano wa Taiwan walikuwa miongoni mwa wengine 35 wa China walionaswa nchini Kenya kwa tuhuma za kumiliki vyombo vya mawasiliano kinyume na sheria za nchi. Ijumaa wiki iliyopita walifikishwa mahakamani mbele ya Hakimu Joyce Gandani kujibu mashtaka yanayowakabili kumiliki na kutumia vyombo hivyo.
Hata hivyo Hakimu huyo aliamuru raia hao kuachiliwa kwa kukosekana ushahidi wa kutosha dhidi ya tuhuma zilizowakabili mbele ya mahakama.Pia Hakimu Gandani aliamuru Kenya kuwarudisha nyumbani mara moja raia hao 35 wa China na watano wa Taiwan.
Lakini Jumatatu Balozi wa Taiwan aliye na makao yake Afrika Kusini akiwa Nairobi wakati watano hao walipofikishwa mahakama aliirai Kenya kuwapeleka raia wake Taipei badala ya Beijing. Kenya nayo kisirisiri ikawapandisha ndege raia hao hadi Beijing bila ya kuzingatia ombia hilo jambo ambalo lilliikera Taiwan. Balozi huyo wa Taiwan John Chen, akizungumza na Sauti ya Amerika kutoka Afrika Kusini, ameisuta serikali ya Kenya kwa kutowaonyesha raia wake heshima.
Lakini Serikali ya Kenya kupitia, Msemaji wa Wizara ya Usalama na Mambo ya Ndani, Mwenda Njoka, Kenya haina uhusiano wowote wa kidiplomasia na Taiwan kwani inaitambua China tu katika mahusiano yake.