Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 22:23

Kenya yasajili simu za mkononi


Matumizi ya simu za mkononi yamezidi nchini Kenya
Matumizi ya simu za mkononi yamezidi nchini Kenya

Kenya imeanza utaratibu wa kusajili simu zote za mkononi nchini humo katika juhudi za kupambana na uhalifu.

Kenya imeanza kazi ya kusajili simu zote za mkononi ikiwa ni miongoni mwa juhudi za kupambana na uhalifu unaotokana na matumizi ya simu hizo.

Watu wanaotaka simu za mkononi watatakiwa kuonyesha hati na anuani za mahali wanapoishi kabla ya kupatiwa namba ya simu. Namba ya simu ambazo itakuwa hazijasajiliwa mpaka mwishoni mwa July zitakatwa, serikali imesema.

Wachambuzi wanasema watu wengi nchini humo wanaunga mkono hatua hiyo ya serikali, kwa matumaini kuwa itasaidia polisi kupambana na uhalifu. Magenge yanayoteka watu nyara katika miji mikubwa mara nyingi yanatumia namba za simu zisizosajiliwa kutuma SMS zinazodai malipo.

Kenya ina watumiaji wa simu za mkononi wapatao millioni 20. Tanzania tayari imeanza zoezi kama hilo la kusajili simu za mkononi.

XS
SM
MD
LG