Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:56

Kenya: Raila na Mudavadi walaumiana hadharani


Musalia Mudavadi (kati kati) akitangaza kujiuzulu kwake kutoka ODM akiwa pamoja na Najib Balala (kulia)
Musalia Mudavadi (kati kati) akitangaza kujiuzulu kwake kutoka ODM akiwa pamoja na Najib Balala (kulia)

Mwishoni mwa wiki Musalia Mudavadi amewataka wananchi wamlazimishe Riala Odinga kustahafu kutoka siasa.

Akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika uwanja wa micghezo wa Nakuru, naibu waziri mkuu Musalia Mudavadi amesema wakati Rais Mwai Kibaki atakapo stahafu kutoka siasa wakati wa uchaguzi basi itabidi Rais pia afuatane nae kwa kutopatiwa kura na wananchi.

Mvutano huo kati ya washirika wa zamani wa muda mrefu ulianza baada ya Bw. Mudavadi kukihama chama cha ODM kinachongozwa na Bw Odinga wiki iliyopita na kujiunga na chama kipya cha UDFP

Akizungumza na Sauti ya Amerika, Bw. Mudavadi amesema anaondoka kutoka ODM kutokana na ukosefu wa demokrasia katika chama hicho na utaratibu wa kupigania nafasi za juu za chama.

makamu huyo wa waziri mkuu anasema chama atakachokitumia kupigania kiti cha rais kitakuwa hakina misingi ya kikabila, kikijumuisha watu wote na kwa njia ya uwazi na demokrasia.

XS
SM
MD
LG