Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 21:01

Kenya: Raila akabiliwa na changamoto ndani ya chama chake


Naibu Wazir Mkuu wa Kenya Musalia Mudavadi (kushoto) akiwa pamoja na Waziri Mkuu Riala Odinga (kulia) wakihudhuria mkutano wa chama cha ODM.
Naibu Wazir Mkuu wa Kenya Musalia Mudavadi (kushoto) akiwa pamoja na Waziri Mkuu Riala Odinga (kulia) wakihudhuria mkutano wa chama cha ODM.

Naibu Waziri Mkuu, Bw Musalia Mudavadi ametangaza atagombania nafasi ya kukiwakilisha chama cha ODM kwenye uchaguzi ujao wa rais.

Uwamuzi huo umewashangaza wengi nje ya chama cha Orange Democratic Movement, ODM, na baadhi kutabiri kwamba huwenda chama kikakabiliwa na msukosuko mkubwa kabla ya uchaguzi mkuu.

Wafuasi wa karibu wa Bw Riala Odinga wameanza kutoa mwito kwa Bw. Mudavadi ajiondowe ili pasiwe na mvutano mkubwa ndani ya chama.

Hii ni mara ya kwanza kwa Waziri Mkuu Raila Odinga kukabiliwa na upinzani wa kweli na mkubwa ndani ya chama chake tangu kuundwa kwa serikali ya mseto nchini Kenya miaka minne iliyopita.

Bw Mudavadi ambae pia ni waziri wa serikali za wilaya, amekua mshauri na miongoni mwa wafuasi wa karibu sana wa Bw. Odinga kwa miaka 15 iliyopita tangu kuundwa kwa chama cha ODM, lakini hivi sasa inaonekana mambo yanabadilika.

Mwanasiasa huyo mkongwe aliyewahi kuwa makamu rais katika serikali ya Rais Daniel Arap Moi, amesema atagombania nafasi ya kukiwakilisha chama katika uchaguzi wa rais, ikiwa ni moja wapo ya utaratibu wa kidemokrasia.

Bw. Mudavadi anasema, "ni lazma tudumishe demokrasia katika chama. Ukishindwa kudumisha demokrasia katika chama utadumisha vipi demokrasia kitaifa."

Licha ya uwamuzi huo Bw Odinga anasema yuko tayari kukabiliana na changamoto hiyo, "kila mtu aliyendani ya chama anahaki na fursa ya kujitetea na kugombani kiti chechote ndani ya chama."

Hata hivyo kuna baadhi ya anachama wanahofia kwamba ikiwa Bw Odinga hatapata ushindi wa kukiwakilisha chama chake basi huwenda akasababisha mgawanyiko katika chama kama alivyowahi kufanya na chama cha KANU.

XS
SM
MD
LG