Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 14:15

Hakuna Mafuta Kenya-Serikali


Vifaa vinavyotumika kuchimba mafuta.
Vifaa vinavyotumika kuchimba mafuta.

Kenya inasema juhudi za kutafuta mafuta kaskazini-mashariki ya nchi hiyo hazikufanikiwa. Miezi kadha iliyopita serikali ya Kenya ilielezea matumaini ya kupata mafuta nchini humo.

Kenya inasema juhudi za kutafuta mafuta kaskazini-mashariki ya nchi hiyo hazikufanikiwa. Miezi kadha iliyopita serikali ya Kenya ilielezea matumaini ya kupata mafuta nchini humo na kutangaza kwamba kampuni ya uchimbaji mafuta ya China, National Offshore Oil, itafanya uchimba wa awali wa mafuta na gesi katika jimbo la North Eastern.

Rais wa Kenya, Mwai Kibaki.
Rais wa Kenya, Mwai Kibaki.

Hata hivyo Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Patrick Nyoike, aliwaambia waandishi wa habari Jumanne, kwamba kampuni hiyo ya China imesitisha uchimbaji bila mafanikio yoyote. Nyoike alisema uchimbaji sasa umefikia kina cha zaidi ya mita elfu tano, na joto kali kwenye urefu huo inamaanisha hakuna uwezekano wa kupata mafuta.

Nyoike alisema serikali itatangaza mwezi ujao kama eneo hilo linaonekana lina gesi. Raia wa Kenya wamekuwa wakitumaini kugunduliwa kwa mafuta sambamba na ugunduzi wa hivi karibuni katika nchi jirani ya Uganda na Tanzania.

XS
SM
MD
LG