Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 22, 2023 Local time: 17:43

Kenya yajikuta katikati ya mvutano wa mkutano wa Kismayo


wanajeshi wa Kenya wakipiga doria katika mji wa Kismayo
Mkutano unaoendelea katika juhudi za kuunda serikali ya majimbo ya Jubba huko kusini mwa Somalia unagubikwa na ugomvi kati ya viongozi wa koo mbali mbali wa majimbo hayo na maafisa wa IGAD.

Mbunge wa zamani wa bunge la Somalia Omar Burale ameiambia Sauti ya Amerika Jumapili kwamba wajumbe kutoka zaidi ya koo 10 wameondoka kutoka mkutano wakidai ukosefu wa utaratibu wa haki katika kuchagua wajumbe watakaomchagua rais mpya wa jimbo hilo.

Akizungumza kutoka Kismayo Bw. Burale anasema “wajumbe wamechaguliwa na maafisa wanaodai ni kutoka Jumuia ya nchi za mashariki na pembe ya Afrika, IGAD, lakini mimi nina amini maafisa hao ni kutoka Kenya wanaompemndelea mmoja kati ya wababe wa vita wa Kismayo Ahmed Madobe.
Mahojiano na Daud Awes - 5:28
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:25 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Hata hivyo kuna afisa kwenye kamati ya matayarisho ya mkutano Kismayo, Abdinasir Gure Farah, anaekanusha ripoti za kuondoka kwa wajumbe kutoka mkutano huo.

Anasema kuna baadhi ya wajumbe wa koo ambao hawajaridhika na jinsi wajumbe walivyochaguliwa, lakini jambo hilo halitoharibu utaratibu wa mkutano anasema.

Katika tukio jingine, mwandishi wa idhaa ya Kisomali Daud Awes anatuarifu kwamba jeshi la Kenya katika mji wa Kismayo limekata ndege yenye ujumbe wa wazee 30 kutoka koo mbali mbali za Juba Land kutuwa.

Kiongozi wa ujumbe huo mbunge wa zamani wa Somalia Mohamed Amin Abdullahi ameiambia Sauti ya Amerika kwamba waliondoka Mogadishu baada ya kupata idhini ya jeshi la Umoja wa Afrika Somalia, AMISOM, na hawajuwi kwanini maafisa wa Kenya walikata ndege yao kutua.

Serikali kuu ya Somalia kwa upande wake unapinga mkutano huo wa Kismayo na viongozi wa IGAD wamemomba rais Hassan Shiekh Mahamud kusimamia utaratibu kamili wqa mkutano huo.
XS
SM
MD
LG