Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 13:46

Watu 3 wafariki kutokana na mafuriko Kenya


Mafuriko yaliyosababishwa na mvua nyingi yamesababisha vifo vya watu watatu na maelfu kupoteza makazi yao. Kulingana na chama cha msalaba mwekundu huko Kenya maafa makubwa yametokea magharibi ya nchi hiyo.

Mafuriko katika sehemu mbali mbali za Kenya kutokana na mvua nyingi yamesababisha vifo vya watu watatu na maelfu kupoteza makazi yao. Chama cha Msalaba Mwekundi huko Kenya kimesema kwamba eneo lililoathirika zaidi ni mkoa wa Turkana ambako vijiji vinne viliharibiwa kutoana na kufurika kwa mto Kalawase.

Mkuu wa jimbo Christopher Musumbu alieleza kwamba serikali imeanza kuwasilisha msaada wa dharura kwa watu walopoteza makazi yao. Kiasi ya watu 1,700 kutoka vijiji 6 katika wilaya ya Marigat pia walipoteza makazi yao kutokana na kufurika kwa mto Endao.

Maafisa wa Msalaba Mwekundu na shirika la misaada la Wold Vison wametembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika na kutoa chakula cha dharura na nyadarua za umbu pamoja na mablanketi.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika Mwai Gikonyo anaripoti kwamba zaidi ya Hekari elfu moja 400 zenye mashamba ya kilimo zimeharibiwa na maji. N a kulingana na utabiri wa hali ya hewa, huwenda mvua zaidi zikaendelea kunyesha katika jimbo la magharibi la Nyanza na kusababisha kufurika kwa mito Nzoia na Yala.

Katika jimbo la kaskazini mashariki, inaripotiwa kwamba daraja muhimu linalounganisha maeneo ya Lodwar na mji wa Lokichogio limeharibiwa kabisa na mafuriko na njia za uchukuzi na mawasiliano zimeharibika.

XS
SM
MD
LG