Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 03, 2022 Local time: 08:53

Kenya yaendelea kukumbwa na changamoto za kiusalama


Polisi mwanamke akiwakagua abiria wanawake wanaosafiri kwenda Nairobi wakitokea Mandera mji mpakani kati ya Kenya na Somalia.

Kenya inakabiliana na matatizo na changamoto za kiusalama katika siku za karibuni hasa kutokana na mashambulizi yanayoaminika kuwa ya kigaidi. Kwa Zaidi ya miaka miwili sasa, jeshi la Kenya limekuwa nchini Somalia ikiwa mojawapo ya juhudi za kubaliana na kundi la wanamgambo wa al-Shaabab ambalo linashukiwa kutekeleza mashambulizi na mauaji nchini .

Hali ya kudorora kwa usalama imeongezeka karibu katika kila pembe ya Kenya huku wasiwasi ukitanda miongoni mwa wananchi wasiojua ni lini au wapi shambulizi lingine litakapotokea. Haya yote yakijiri, viongozi na mafisa wa usalama wanaendelea kunyoosheana vidole vya lawama na kutoa mapendekezo tofauti ya jinsi ya kuboresha usalama.

Eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya limeshuhudia mashambulizi na hasa kaunti ya Mandera ambapo makumi ya watu wameuliwa na wengine wengi kujeruhiwa kwenye mashambulizi tofauti. Gavana wa eneo hilo Ali Roba ameshambuliwa kwa zaidi ya mara sita sasa na swala hili limemshawishi kutoa mapendekezo kadhaa yakiwemo kubadilishwa kwa utawala wa jeshi la polisi katika kaunti ya Mandera.

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya VOA, Msomi ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya kisaikolojia katika chuo kikuu cha USIU kilichoko Nairobi, Dr Oscar Wanyutu, anaelezea hatua gani zinaweza kuchukuliwa ili kuwaondolea khofu ya usalama wakazi wa Mandera ambao wamekuwa wakiishi katika hali ya wasi wasi.

please wait
Embed

No media source currently available

0:00 0:05:57 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG