Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 02, 2022 Local time: 01:03

IAAF yawasimamisha maafisa 3 wa riadha Kenya


Kenyan athletes protesting Athletics Kenya

Maafisa watatu wa ngazi za juu katika chama cha riadha nchini Kenya - Athletics Kenya - wamesimamishwa na na shirikisho la riadha duniani - IAAF - kufuatia madai ya kukwepa utaratibu wa kuzuia madawa ya kuongeza nguvu katika riadha na kuchukua fedha kutoka kampuni ya Nike.

Rais wa Athletics Kenya Isaiah Kiplagat amesimamishwa uongozi kwa siku 180 na ameambiwa pia kuna madai dhidi yake kuhusu "zawadi" ya magari mawili kutoka kwa shirikisho la riadha la Qatar.

Kiplagat anashutumiwa kwa kujipatia magari hayo binafsi au kwa ajili ya shirikisho la Qatar ambalo litakuwa mwenyeji wa mashindano ya dunia 2019. Qatar haijatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.

IAAF inasema imewasimamisha pia makamu rais wa Athletics Kenya David Okeyo na kiongozi wa timu ya kenya katika mashindano ya dunia mwaka 2015 Joseph Kinyua wakati uchunguzi ukiendelea.

Madai hayo yanakuja huku kukiwa na ufuatiliaji makini wa ongezeko la matukio ya karibuni wanariadha 40 wa Kenya kufeli katika vipimio vya madawa ya kuongeza nguvu tangu mwaka 2012

XS
SM
MD
LG