Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 13, 2025 Local time: 00:38

Keir Starmer wa Uingereza amethibitisha serikali yake haitatekeleza sera za nyuma


Waziri Mkuu Mpya wa Uingereza, Keir Starmer
Waziri Mkuu Mpya wa Uingereza, Keir Starmer

Serikali yake haitatekeleza sera ya mtangulizi wake kuwahamisha waomba hifadhi wanaowasili Uingereza na kupelekwa Rwanda.

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amethibitisha leo Jumamosi kuwa serikali yake mpya haitatekeleza sera ya mtangulizi wake ya kuwahamisha waomba hifadhi wanaowasili nchini humo katika boti ndogo na kupelekwa Rwanda, na kusitisha mpango huo kabla ya ndege yoyote kuanza kuondoka.

“Mpango wa Rwanda ulikuwa umekufa na kuzikwa kabla ya kuanza. Haijawahi kutokea kuwa kizuizi kwa boti ndogo,” Starmer alisema katika mkutano na waandishi wa habari.

“Siko tayari kuendelea na hatua hii kama kizuizi”.

Forum

XS
SM
MD
LG