Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 21:49

Trump: Kauli ya McCain 'Inawapa Maadui Nguvu'


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump amemshukia Seneta wa Republikan John McCain katika ujumbe wa Twitter Alhamisi, akisema kuwa ukosoaji wake "unawapa maadui nguvu."

McCain amekosoa shambulizi la kijeshi lililofanywa Yemen ambapo askari wa jeshi la majini wa Marekani aliuawa.

Seneta McCain alielezea Jumatano shambulizi hilo lililofanyika wiki iliyopita, na kumuua mkuu wa operesheni maalum ya kivita William “Ryan” Owens, lilikuwa halina mafanikio yoyote.

McCain amesema shambulizi hilo, ambalo lilisababisha vifo vya raia, wakiwemo watoto wadogo na wanawake, na pia hasara kubwa ya dola milioni 75 kutokana na ndege hiyo kuanguka na kuharibika kabisa, “haiwezi kuitwa ni mafanikio.”

Msemaji wa White House Sean Spicer ametetea shambulizi hilo Jumatano, akisema liliwaua washukiwa karibuni 14 waliokuwa wakishirikiana na al-Qaida.

Shambulizi hilo ni la kwanza katika operesheni ya kupambana na ugaidi tangu uongozi mpya wa Trump uchukue madaraka.

Shambulio hilo liliwalazimisha serikali ya Yemen kusema Jumatano ilikuwa imeomba shambulio hilo lifanyiwe tathmini upya na kukanusha repoti zinazodai kuwa Yemen iliomba mpango wa kupambana na ugaidi kwa kushirikiana na Marekani usitishwe.

"Yemen inaendelea kushirikiana na Marekani na inaheshimu mikataba yote," amesema Waziri wa Mambo ya Nje Abdul-Malik al-Makhlafi huko Cairo.

Pia amesema "sio kweli" kwamba Yemen imeitaka Marekani kusitisha operesheni maalum.

McCain ambaye mara nyingi amekuwa akimkosoa rais, ni mwanajeshi mstaafu aliyewahi kushiriki katika vita ya Vietnam na pia kuwa mfungwa wa kivita.

Baada ya kushindwa uchaguzi wa urais 2008 alipochuana na Barack Obama, McCain alichaguliwa tena kuwa seneta wa Jimbo la kusinimagharibi ya Arizona.

XS
SM
MD
LG