Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 21:40

Katika kuadhimisha siku ya TB duniani, WHO yatoa wito wa kuchukuliwa hatua ili kuondoa janga


Timu za Huduma ya Afya ya UKIMWI (AHF), ambazo zimeweka kipaumbele katika upimaji wa TB katika kliniki—pamoja na kuzuia na kutibu maambukizo ya VVU/TB—zinafanya maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani kote, (Business Wire)
Timu za Huduma ya Afya ya UKIMWI (AHF), ambazo zimeweka kipaumbele katika upimaji wa TB katika kliniki—pamoja na kuzuia na kutibu maambukizo ya VVU/TB—zinafanya maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani kote, (Business Wire)

Katika kuadhimisha Siku ya Kifua Kikuu Duniani, Shirika la Afya Duniani-WHO  linatoa wito wa kuchukuliwa hatua ili kuondoa janga hili  ambalo limekuwa limeumiza  na kuuwa mamilioni ya watu katika miaka kadhaa.

Kauli mbiu ya mwaka huu, “Ndiyo! Tunaweza kukomesha TB,” inakusudiwa kutuma ujumbe wa matumaini kwamba kukomesha janga hilo, ambalo WHO linasema kila mwaka husababisha vifo vya takriban watu milioni 1.3, kunawezekana.

Wakati ugonjwa huo unatibika na kuzuilika, wakuu wa nchi katika mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu TB wa mwaka 2023 walikadiria kuwa dola bilioni 13 zilihitajika kila mwaka kwa ajili ya kuzuia, utambuzi, matibabu, na matunzo ili kukomesha janga hilo ifikapo mwaka 2030.

Wakuu wa nchi, ambao waliahidi kuharakisha maendeleo ili kukomesha TB na kugeuza ahadi hizi kuwa vitendo vinavyoonekana, waliidhinisha mfululizo wa malengo ya kimataifa ya kusogeza mchakato huu mbele.

Forum

XS
SM
MD
LG