Guterres ameziambia nchi wanachama wa Umoja wa mataifa “Vitisho vipya vya leo kwa amani vinaleta maombi mapya kwetu.”
Amesema mapendekezo yake yaliyofafanuliwa katika maelezo mafupi ya sera inayoitwa “Ajenda mpya ya amani,” yanatambua hali ya kuunganishwa kwa changamoto nyingi za kimataifa.
“Mizozo imekuwa tete, mibaya na migumu kusuluhisha,” amesema.
Ameongeza kuwa “mwaka uliopita ulishuhudia idadi kubwa ya vifo vinavyohusishwa na mizozo katika kipindi cha miongo mitatu.”
Amesema Uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine umefanya kuwa vigumu kutatua changamoto nyingi za kimataifa.
“Ikiwa kila nchi itatekeleza wajibu wake chini ya mkataba wa Umoja wa mataifa, haki ya kupata amani itahakikishwa”, Guterres amesema.
Ameongeza kuwa nchi zinapokiuka ahadi hizo, zinaunda ulimwengu usiokuwa na amani kwa kila mtu.
Forum