Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 01:12

Katibu mkuu wa NATO: Vita vya Ukraine vyaweza kudumu miaka mingi


Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akifanya mkutano na waandishi wa habari kabla ya mkutano maalum wa mawaziri wa ulinzi wa NATO, kufuatia uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine, Brussels, March 15, 2022. Picha ya Reuters
Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akifanya mkutano na waandishi wa habari kabla ya mkutano maalum wa mawaziri wa ulinzi wa NATO, kufuatia uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine, Brussels, March 15, 2022. Picha ya Reuters

Vita vya Russia dhidi ya Ukraine vinaweza vikadumu miaka kadhaa, katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ameonya Jumapili, lakini amesema washirika wa nchi za magharibi hawapaswi kupunguza uungwaji mkono kwa vikosi vya Kyiv.

"Tunapaswa kujiandaa kwa kuzingatia kuwa vitadumu miaka kadhaa," Stoltenberg ameliambia gazeti la Ujerumani Bild am Sonntag. "Hatupaswi kuacha kuiunga mkono Ukraine, hata kama gharama ni kubwa, sio tu kwa msaada wa kijeshi, pia kwa sababu ya kupanda kwa bei ya nishati na chakuka."

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson, ambaye alifanya ziara mjini Kyiv siku ya Ijumaa na kuahidi mafunzo kwa wanajeshi wa Ukraine, alionya dhidi ya kuchoshwa na hali ya Ukraine wakati vita vya Ukraine vinaelekea kwenye mwezi wa nne siku zijazo.

Katika maoni yake yaliyochapishwa na gazeti la London Sunday Times, Johnson alisema ni kuhakikisha "Ukraine inapata silaha, vifaa, zana za kijeshi na mafunzo kwa haraka zaidi kuliko mvamizi."

XS
SM
MD
LG