Rais Joe Biden alisema siku ya Alhamisi amemchagua Karine Jean-Pierre kuwa Msemaji wa White House, anamrithi Jen Psaki na kuwa mtu wa kwanza mweusi na wa mapenzi ya jinsia moja kuhudumu kama uso wa umma wa serikali ya Marekani.
Psaki, ambaye anaacha kazi hiyo Mei 13, alikuwa amekwishasema mapema katika utawala wa Biden, ulioanza Januari 2021, kwamba alipanga kukaa kwa takriban mwaka mmoja.
Jean-Pierre amehudumu kama naibu msemaji wa White house tangu mwanzo wa muhula wa Biden. Alifanya kazi katika kampeni yake ya urais 2020, katika Ikulu ya Rais Barack Obama, na alikuwa afisa mkuu wa masuala ya umma wa MoveOn.org, taasisi ya utetezi ya wanaharakati.
Facebook Forum