Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:56

Kanisa Katoliki lapata Baba Mtakatifu mpya


Baba Mtakatifu mpya Francis I (Kati) akionekana kwa mara ya kwanza muda mfupi baada ya kuchaguliwa huko Vatican, Mar 13, 2013.
Baba Mtakatifu mpya Francis I (Kati) akionekana kwa mara ya kwanza muda mfupi baada ya kuchaguliwa huko Vatican, Mar 13, 2013.
Kadinali mwenye asili ya Argentina Jorge Mario Bergoglio amechaguliwa kuwa Baba Mtakatifu wa 226 wa kanisa katoliki akichukua nafasi ya baba mtakatifu benedict ambaye alijiuzulu mwezi uliopita.

Makadinali 115 walioshiriki utaratibu wa kumchagua Baba Mtakatifu mpya kwenye chuo cha makadinali walimchagua Baba Mtakatifu mpya mwenye umri wa miaka 76 Jumatano jioni kwa saa za Vatican kwenye siku ya pili ya utaratibu wa kupiga kura kumpata kiongozi mpya wa kanisa katoliki. Baba Mtakatifu mpya amechagua jina la Francis I.

Mgombea alitakiwa kupata theluthi mbili ya kura au asilimia 77 ili aweze kuchaguliwa kuwa kiongozi wa wakatoliki duniani.

Maelfu ya watu walikusanyika kwenye uwanja wa St. Peters huko Vatican kushuhudia tangazo la kihistoria.

Moshi mweupe ulitokea katika tanuri kwenye kanisa dogo la Sistine na kengele ziligonga kwenye mji wa Vatican City Jumatano jioni zikiashiria kuwa Baba Mtakatifu mpya amechaguliwa kuongoza waumini wa kikatoliki bilioni 1.2 duniani.

Makadinali ambao wote walikuwa chini ya umri wa miaka 80 walianza kupiga kura za kumchagua Baba Mtakatifu mpya siku ya Jumanne. Kama ilivyotarajiwa kura ya kwanza haikuzaa matunda lakini huwenda ilitoa mwongozo wa kupatikana kwa Baba Mtakatifu. Kura ya Jumatano asubuhi pia haikuzaa matunda.

Makadinali wote 115 walioshiriki katika utaratibu wa kumchagua Baba Mtakatifu mpya walikula kiapo cha kutunza siri kwa muda wote wa utaratibu wa kumchagua Baba Mtakatifu hadi zoezi hilo litakapokamilika na kumpata kiongozi mpya wa kanisa la katoliki duniani.
XS
SM
MD
LG