Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 13:05

Kampuni zaomba kuanza kutumia chanjo dhidi ya Corona


Kampuni ya kutengeneza dawa ya Moderna imesema kwamba inataka idhini ya dharura kwa ajili ya kutumia chanjo yake dhidi ya virusi vya Corona hapa nchini Marekani na Ulaya.

Hii ni baada ya chanjo hiyo kuonyesha ufanisi wa asilimia 94.

Ombi hilo lina maana kwamba maafisa wa afya wanaweza kutumia chanjo hiyo kuanzia katikati mwa mwezi Desemba.

Kampuni ya Moderna imesema kwamba imekamilisha kufanyia majaribio chanjo hiyo, kati ya watu 30,000 na matokeo yake yalikuwa mazuri sana.

Hatua ya kampuni za Modern ana Pfizer kuomba kuanza kutumia chanjo yake kwa matumizi ya dharura, inajiri wakati idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani ikiwa inaongezeka kwa kasi sana.

Maelfu ya watu wanagunduliwa kuambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani kila siku.

Maafisa wa afya wameeleza wasiwasi kwamba idadi ya maambukizi huenda ikaongezeka zaidi kwa sababu watu wamekataa kuzingatia maagizo ya afya kuzuia maambukizi.

Maambukizi yaongezeka kwa kasi Marekani, Brazil na Mexico

Wakati huo huo shirika la afya duniani WHO limesema kwamba lina wasiwasi sana kutokana na kuongezeka haraka kwa idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya Corona nchini Brazil na Mexico.

Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amewaambia waandishi wa habari kwamba Brazil inastahili kuchukua hatua za haraka sana kukabiliana na maambukizi.

Ametoa wito sawa na huo kwa viongozi nchini Mexico, akisama kwamba hali nchini humo ni mbaya sana.

Amesema kwamba idadi ya watu ambao wameambukizwa na wale ambao wamefariki kutokana na Corona imeongezeka mara mbili zaidi na kutaka viongozi wa Mexico kuchukua hatua Madhubuti kwa haraka.

Jumla ya watu 100,000 wamefariki kutokana na Corona nchini Mexico kufikia Novemba 20. Kwa jumla, watu 5,000 wamefariki nchini humo.

Nchini Brazil, watu 172,000 wamefariki na kuifanya kuwa nchini ya pili kurekodi idadi ya juu ya vifo kutokana na Corona baada ya Marekani ambayo imerekodi vifo vya watu 267,000.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG