Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 07:13

Kampuni ya nishati Libya inasema usalama umeimarika nchini humo


Mfano wa kiwanda cha mafuta cha Ras Lanuf cha Libya. Oct. 19, 2019
Mfano wa kiwanda cha mafuta cha Ras Lanuf cha Libya. Oct. 19, 2019

NOC katika ombi lake ilifuata  uchambuzi wa kweli na wa kimantiki wa hali ya usalama ambao umeanza kuimarika kwa kiasi kikubwa nchini Libya

Kampuni ya taifa ya nishati nchini Libya imewasihi washirika wake wa kigeni wa mafuta na gesi kuanza tena utafutaji na uzalishaji siku ya Jumanne ikiwahakikishia usalama umeanza kuimarika kwa kiasi kikubwa baada ya mapigano mapema mwaka huu.

Tawala hasimu mashariki na magharibi zimekuwa zikigombea madaraka tangu mwezi Machi katika mvutano ambao umedumaza juhudi za Libya za kuongeza pato kwa kiasi kikubwa ikiwa ni majibu kwa ongezeko la mahitaji ya Ulaya ya mafuta na gesi isiyo ya Russia.

"Shirika la Taifa la Mafuta linatoa wito kwa makampuni ya kimataifa ya mafuta na gesi ambayo yamesaini mikataba ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi kuondoa makampuni waliyotangaza" kampuni hiyo ilisema katika taarifa.

Hatua hiyo ya kisheria inayaruhusu makampuni kujiondoa yenyewe kutoka katika majukumu ya kimkataba kwa kuzingatia mazingira yaliyo nje ya uwezo wao.

NOC katika ombi lake ilifuata uchambuzi wa kweli na wa kimantiki wa hali ya usalama ambao umeanza kuimarika kwa kiasi kikubwa.

Kampuni hiyo ilielezea "utayari wa kutoa msaada wowote muhimu ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira salama ya kufanya kazi kwa kushirikiana na mamlaka za kiraia na kijeshi."

XS
SM
MD
LG