Vitengo vitatu vya BGI ni miongoni mwa makampuni ya China yalioordheshwa wiki iliyopita na Marekani kwamba yanazuia ukaguzi wa kitekonlojia wa Marekani kwa misingi ya kiusalama au haki za binadamu.
Wizara ya biashara ya Marekani imeangazia hatari iliyopo kutoka kwa teknolojia ya BGI katika kuchangia ujasusi wa China. Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kwamba Beijing inajaribu kubuni mtandao wenye taarifa za kijenetiki kutoka kwa waislamu pamoja na makundi mengine ya walio wachache nchini China.
Serikali ya China Ijumaa wiki iliyopita ililalamikia Washington kwa kulenga makampuni yake bila sababu. BGI yenye makao yake makuu kwenye mji wa kusini mwa China wa Shenzhen, imesema kwamba inajishugulisha na huduma za kijamii na kisayansi pekee.
Facebook Forum