Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:52

Waasi wa Syria wautwa uwanja wa ndege


Kambi ya jeshi la anga, karibu na Al-Bukamal, Syria
Kambi ya jeshi la anga, karibu na Al-Bukamal, Syria

Wapiganaji wa waasi wa Syria wanaosaidiwa na Marekani wamechukua udhibiti wa uwanja mdogo wa ndege uliotumika kama kambi na kundi la Islamic State karibu na mpaka wa Irak mapema leo Jumatano.

Kambi ya jeshi la anga huko Hamdan ilitumika kama kituo muhimu cha kijeshi cha Islamic State karibu na mji wa Al-Bukamal, kilomita chache kutoka Irak.

Kambi hiyo ya jeshi la anga ilitekwa saa kadhaa baada ya kuanzishwa mashambulizi jana Jumanne yaliyokuwa na lengo la kufunga njia inayotumiwa na kundi la ugaidi kuingia Syria na Irak.

Kundi la Islamic State lilichukua udhibiti wa Al-Bukamal mwaka 2014 kwa ajili ya operesheni zao za kijeshi na mara moja kuondoa mpaka kati ya Irak na Syria.

XS
SM
MD
LG