Taarifa iliyotiwa saini na mkuu wa jeshi imesema kwamba jeshi lilihitaji kumlinda rais na familia yake, wakati likizuia mapambano mabaya ambayo huenda yakapelekea umwagaji damu na kuathiri usalama wa raia.
Rais Mohamed Bazoum na waziri wa mambo ya kigeni Hassoumi Massoudou, mapema waliyaomba makundi ya kidemokrasia nchini kukemea mapinduzi hayo, wakati maafisa kutoka mataifa ya Magharibi wakisema kwamba jaribio hilo la mapinduzi halieleweki.
Taarifa iliyotolewa na jeshi Jumatano usiku kwa njia ya televisheni ilisema kwamba Bazoum alikuwa amepokonywa madaraka na kwamba taasisi za serikali zimesitishwa, yakiwa mapinduzi ya 7 huko Afrika Magharibi na Kati tangu 2020.
Bazoum kupitia ujumbe kwenye mitandao ya kijamii mapema Alhamisi ameapa kulinda mafanikio ya kidemokrasia katika nchi ambayo ni mshirika muhimu kwa mataifa ya magharibi, yanayosaidia kupambana na uasi katika eneo la Sahel.
Forum