Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:25

Kamanda wa juu wa al-shabab akamatwa


Wanamgambo wa Al-Shabab
Wanamgambo wa Al-Shabab

Maafisa wa Somalia wanasema wamemkamta mmoja wa makamanda wa juu ya kundi la Al-Shabab. Zakariye Ismail Hersi alikamatwa katika uvamizi uliofanywa Jumamosi katika mji wa El Wak karibu na mpaka wa Kenya.

Kamanda wa jeshi la Somalia Jenerali Abbasi Ibrahim Gurey anayesimamia shughuli za kijeshi katika eneo la Gedo kusini mwa Somalia, aliiambia idhaa ya Kisomali ya Sauti ya Amerika kuwa maafisa walipashwa habari na wananchi kwamba kuna wanamgambo wa al-Shabab waliokuwa wakijificha katika nyumba moja ya eneo hilo.

Jenerali Gurey alisema Hersi alikamatwa pamoja na msaidizi wake. Alisema kuwa Hersi ambaye alikuwa na bunduki hakupigana na wanajeshi wakati wa kukamatwa kwake.

Juni mwaka 2012, Marekani ilitangaza zawadi ya dola milioni 3 kwa yeyote atakayemkamata Hersi, ikimwelezea kama mshirika wa karibu wa kiongozi wa zamani wa al-Shabab Ahmed Abdi Godane.

Hersi alisema hakuwa na habari kwamba Marekani ilikuwa imetangaza zawadi ya mamilioni ya dola kwa kukamatwa kwake.

Alisema hajawahi kuwa mkuu wa maswala ya kijasusi wa Al-Shabab kama ilivyoripotiwa awali lakini alitumika katika nyadhifa nyingine ikiwemo kuwa mkuu wa utawala wa maeneo kadhaa na mmoja wa makamanda wa kundi hilo la al-Shabab.

XS
SM
MD
LG