Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 16, 2025 Local time: 07:19

Kamanda wa ADF anahusishwa na mashtaka ya mauaji ya watalii na wengine

Uganda inalilaumu kundi la ADF ambalo lina uhusiano na kundi la Islamic State kwa mauaji ya watalii waliokuwa kwenye fungate, wakiwa na muongozaji wao katika eneo pamoja na shambulio la shule lililosababisha vifo vya watu 42, wengi wao wakiwa wanafunzi.

Waendesha mashtaka nchini Uganda wamemfungulia mashtaka kamanda wa kundi la wanamgambo wanaohofiwa kwa ugaidi na mauaji ya watalii wawili wa kigeni pamoja na dereva wao mwezi uliopita.

Kamanda katika kundi la wanamgambo wa Allied Democratic Forces (ADF), Abdul Rashid Kyoto, maarufu kama Njovu alikamatwa mwanzoni mwa mwezi huu na pia anatuhumiwa kuongoza mauaji ya kutisha katika shule moja hapo mwezi Juni.

Uganda inalilaumu kundi la ADF ambalo lina uhusiano na kundi la Islamic State kwa mauaji ya watalii waliokuwa kwenye fungate, wakiwa na muongozaji wao katika eneo pamoja na shambulio la shule lililosababisha vifo vya watu 42, wengi wao wakiwa wanafunzi.

Waendesha mashtaka wamefungua mashtaka mawili ya ugaidi, mashtaka matatu ya mauaji, mashtaka matatu ya wizi wa kutumia nguvu na shtaka moja la kuhusika na kundi la kigaidi, kuhusiana na shambulio hilo la kitalii, mkurugenzi wa mashtaka ya umma alisema katika taarifa Jumatatu.

Forum

XS
SM
MD
LG