Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 16:12

Kagame kuhudhuria ufunguzi wa Kombe la Dunia Russia


Rais Paul Kagame wa Rwanda

Rais Paul Kagame wa Rwanda atahudhuria ufunguzi wa michuano ya fainali za kombe la dunia, Alhamisi, huko Russia.

Kwa mujibu wa gazeti la Rwanda “Kigali today”, Rais Kagame atahudhuria sherehe za ufunguzi wa mashindano kwa niaba ya Umoja wa Afrika, kama mwenyekiti wa umoja huo .

Bara la Afrika limewakilishwa kwenye kombe hilo na timu tano ambazo ni Nigeria, Tunisia, Senegal, Misri na Morocco.

Rais Kagame alikutana Jumatano na Rais wa Russia Vladimir Putin, mjini Moscow.

Kwa mujibu wa gazeti la Rwanda “New times”, Rwanda itapokea mwaka huu mkutano wa nane wa baraza la shirikisho la soka duniani FIFA, unaotarijiwa kufanyika tarehe 25 na 26 mwezi Oktoba.

Russia ni mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Dunia 2018 yaliyopangwa kuanza Alhamisi wiki hii.

Viongozi hao wawili wamekutana katika kipindi chini ya wiki mbili baada ya Waziri Mkuu wa Russia, Sergey Lavrov kutembelea Kigali.

Wakati wa ziara yake nchi hizo mbili zimeahidi kuimarisha uhusiano wao katika nyanja za ulinzi, kilimo na elimu kati ya maeneo mengine mengi.

Rais Kagame ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika hivi sasa, pia alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje Lavrov Kigali. Hivi sasa nchi hizo mbili zinaandaa makubaliano ya ushirikiano.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG