Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 22:40

Kagame asema hatagombea urais Rwanda 2017


Rais wa Rwanda, Paul Kagame
Rais wa Rwanda, Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame anasema hana nia ya kuwania muhula wa tatu wa urais wakati muhula wake utakapoisha mwaka 2017.

Bwana Kagame alivilaumu vyombo vya habari Jumatano kwa kuanzisha mdahalo iwapo yeye Kagame atakiuka katiba ya nchi na kuwania urais kwa muhula mwingine.

Februari 8, Kagame alikutana na kamati ya viongozi wa juu kitaifa wa chama chake na aliwaelekeza kupanga njia za kusonga mbele kwa nchi baada ya mwaka 2017 na kuzusha hisia kuwa alikitaka chama kuchanganua namna ataweza kuhudumu muhula wa tatu.

Katika mkutano na waandishi wa habari Jumatano Kagame alisema hana nia ya kuongoza muhula mwingine.

Chama kimoja cha upinzani cha siasa cha FDU-Inkingi kilisema katika taarifa yake wiki hii kwamba kililaani mbinu zozote zinazofanywa na Kagame kubadilisha katiba na kuwania urais kwa muhula wa tatu.
XS
SM
MD
LG