Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 14:47

Kaburi la pamoja la watu 18 lagundulika Libya


Serekali ya Libya, Jumapili imesema wamegundua miili 18 ya watu waliozikwa kwenye kaburi la pamoja katika mji wa kati  wa pwani wa Sirte.

Mji huo ni ngome ya zamani ya kundi la Islamic State katika taifa hilo la Afrika Kaskazini lililokumbwa na migogoro.

Mamlaka ya Watu Waliopotea ilisema katika taarifa yake miili hiyo ilifukuliwa katika eneo la Sabaa, kabla ya kuchukuliwa na kupelekea hospitali ya Ibn Sina mjini Sirte.

Sirte, ni sehemu alikozaliwa diktetea wa muda mrefu wa Libya, Moammar Gadhafi, na iliangukia chini ya udhibiti wa wanamgambo wa Islamic State kati ya 2015 na 2016.

Wanamgambo hao, pamoja na al-Qaida, walipata nafasi ndani ya Libya yenye utajiri wa mafuta katikati ya machafuko yaliyoikumba nchi hiyo baada ya uasi wa 2011 na uingiliaji wa NATO katika mzozo huo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG