Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:21

Kabila asema uchaguzi DRC utafanyika 'karibuni'


Rais Joseph Kabila wa DRC ahutubia kikao cha 72 cha umoja wa Mataifa mjini New York.
Rais Joseph Kabila wa DRC ahutubia kikao cha 72 cha umoja wa Mataifa mjini New York.

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Jumamosi alisema kwamba tarehe ya uchaguzi wa urais ambao umekuwa ukisubiriwa kwa hamu na wadau, itatangazwa hivi 'karibuni.'

Kabila alisema kuwa DRC inajitayarisha kwa mchakato wa uchaguzi huo, na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuiunga mkono nchi hiyo, ikielekea kwa zoezi hilo ambalo limeibua mzozo wa kisiasa.

Akizungumza kwenye kikao cha baraza la umoja wa mataifa mjini New York, Marekani, rais huyo alisema kuwa tayari watu milioni 42 kati ya milioni 45 ambao wanatarajiwa kupiga kura, wamesajiliwa. Alisema uasili wa kupiga kura unaendelea katika eneo lililokumbwa na vurugu la Kasai.

Hata hivyo, tume ya uchaguzi nchini Kongo imesema kuchelewa kwa zoezi la usajili wa wapijai kura katika jimbo la Kasai kutachelewesha uchaguzi huo na hautaweza kufanyika mwaka huu.

Serikali na upinzani zilikuwa zimekubaliana kufanyika kwa uchaguzi huo mwezi Desemba mwaka huu, na upinzani umemshutumu Kabila kwamba aknachelewesha zoezi hilo kimakusudi.

Kabila aidha alikosoa Umoja wa Mataifa na kusema kuwa ujumbe wa MUNUSCO, haupaswi kwendelea kuwa nchini mwake bila kujulikana utaondoka lini.

Rais huyo huyo pia amesema kwamba DRC iko tayari kutekeleza wajibu wake kuhusiana na mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Paris.

XS
SM
MD
LG