Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 09:04

Rais mstaafu wa Zanzibar Aboud Jumbe Mwinyi afariki dunia


Makamu Rais wa Tanzania Aboud Jumbe akimpokea Samuel Doe kiongozi wa Liberia mjini Dar es salaam 1980

Rais mstaafu wa awamu ya pili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia Jumapili saa saba mchana nyumbani kwake katika kijiji cha Mji Mwema, eneo la kigamboni jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bwana Mohamed Aboud, mwili wa Mzee Aboud Jumbe Mwinyi ambaye pia alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajiwa kusafirishwa Jumatatu kwa ndege kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya maziko.

Bwana Mohamed Aboud amesema Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake eneo la Migombani, Mkoa wa Mjini Maghrib mnamo saa saba za mchana. Marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka 96 alizaliwa June 14, 1920 huko Juba, Sudan Kusini.

Aidha viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanatarajia kuhudhuria maziko hayo ya Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi .

Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi alishika wadhifa wa Rais wa Zanzibar April 7, 1972 mara tu baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa kwanza wa visiwa hivyo Abeid Amani Karume. Hayati Aboud Jumbe alijiuzulu urais wa Zanzibar pamoja na nyadhifa nyingine za makamu mwenyekiti wa CCM na makamu rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Januari 30, 1984.

Mungu alizale roho ya Marehemu mahali pema peponi

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG