Mjumbe maalum wa Marekani kwa Sudan, Tom Perriello amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Jumatatu kwamba kutokana na udharura wa mgogoro wa Sudan, wajumbe kutoka Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Misri, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu wamekuwa wakifanyiakazi masuala yanayohusiana na usaidizi wa misaada ya kibinadamu na ulinzi wa raia.
“Pamoja na wadau wa masuala ya kibinadamu na wanadiplomasia kote ulimwenguni, sasa tuko kwenye ukingo wa Adre ukiwa wazi na zaidi ya malori 100 yakitarajiwa kuingia mapema kesho,” amesema.
Forum