Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 06:21

Watu 15 Geita wakutwa hai baada ya kufukiwa na kifusi


Mmoja wa wachimbaji akitolewa kutoka kwenye kifusi
Mmoja wa wachimbaji akitolewa kutoka kwenye kifusi

Watu wote 15 wamekutwa hai na vikosi vilivyokuwa vikiwatafuta baada ya kufukiwa na mgodi katika eneo la uchimbaji dhahabu la RZ union uliyopo Nyarugusu Mkoani Geita.

VIKOSI vimefanikiwa kuwafukua wachimbaji baada kuchimba umbali wa mita 30 na kuwakaribia.

Waokoaji wafanikiwa kuwatoa wachimbaji 15
Waokoaji wafanikiwa kuwatoa wachimbaji 15

Juhudi za kuwatafuta watu hawa waliofukiwa zilianza tangu Jumatano chini ya usimamizi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Ofisi ya Madini Kanda ya Ziwa Magharibi ikishirikisha kampuni za migodi GGM na Busolwa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga, amewaonya wawekezaji wa migodi mkoani Geita hasa wanaoendesha uchimbaji kuzingatia kanuni za usalama hivyo.

XS
SM
MD
LG