Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 18:24

Juhudi za kuachiliwa mateka zaidi wanaoshikiliwa Gaza zinaendelea


Wapalestina wakiharakisha kuchukua maji yaliyodondoka kutoka katika lori lililokuwa limebeba msaada wa kinadamu wakati likipita eneo la Rafah huko kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februaryi 18, 2025.
Wapalestina wakiharakisha kuchukua maji yaliyodondoka kutoka katika lori lililokuwa limebeba msaada wa kinadamu wakati likipita eneo la Rafah huko kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februaryi 18, 2025.

Juhudi za kuwaachilia mateka wanaoshikilia na wanamgambo wa Hamas, zinaendelea ili kuhakikisha kwamba wanaachiliwa wote wiki hii.

Hayo ni kulingana na afisa katika serikali ya Israel.
Hatua hiyo ni ya awamu ya kwanza ya kutimiza makubaliano ya kumaliza vita kati ya Israel na Hamas.
Kati ya mateka 33 wanaotarajiwa kuachiliwa chini ya awamu ya kwanza ya makubaliano hayo, 19 wameachiliwa tayari na Israel imesema kwamba nane wamekufa.
Hii inamaana kwamba mateka sita ndio wataachiliwa katika awamu hii.
Afisa katika serikali ya Israel ameambia shirika la habari la AFP kwamba Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu anafanya kila juhudi kuhakikisha kwamba mateka sita walio hai wanaachiliwa huru wiki hii.
Afisa wa Palestina amesema wafungwa watabadilishana na mateka, Jumamosi hii.

Forum

XS
SM
MD
LG