Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 10:52

Jordan yajaribu kufufua mazungumzo ya Mashariki ya Kati


Mfalme Abdullah wa Jordan, (kushoto), na rais Mahamoud Abbas wa Palestina mjini Ramallah ukingo wa Magharibi.
Mfalme Abdullah wa Jordan, (kushoto), na rais Mahamoud Abbas wa Palestina mjini Ramallah ukingo wa Magharibi.

Mazungumzo ya utaratibu wa amani kati ya Wapalestina na Waisrael, yamekwama kutokana na kuendelea ujenzi wa makazi ya walowezi kwenye ukingo wa Magharibi.

Wapatanishi wa Israel na Palestina wanakutana Jumatatu mjini Amman kwa mazungumzo yasiyo rasmi. Hata hivyo wajumbe kutoka pande zote watatafuta njia za kuanza tena mazungumzo ya amani ambayo yamekwamaa kutokana na ujenzi wa makazi ya walowezi na Israel huko Ukingo wa Magharibi.

Wapatanishi watakutana na ujumbe wa wapatinishi wa Ujumbe wa pande nne wa Mashariki ya kati, Quartet, ambao ni Marekani, Umoja wa Ulaya, Russia na Umoja Mataifa. Ujumbe huo umezipatia Israel na utawala wa Palestina hadi Januari 26, kuwasilisha mapendekezo juu ya mipaka na usalama mambo ambayo yatafungua njia ya kuanza tena mazungumzo.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbass anasema muda unayoyoma, akionya kwamba ikiwa hakuna makubaliano yatafikiwa katika tarehe ilowekwa ya Januari 26, basi kazi za ujumbe wa Quartet zitakuwa zimeshindwa na Wapalestina watawajibika kuchukuwa hatua zinazohitajika.

Anasema wakati yeye anapinga ghasia, lakini kuna wito unoongezeka mionogoni mwa Wapalestina kufanya intifada ya tatu dhidi ya Israel.

Suala kuu linaloendelea kukwamisha mazungumzo na kusababisha Wapalestina kutoweza kurudi kwenye meza ya majadiliano ni kukata kwa Israel kusitishe ujenzi wote wa makazi ya walowezi.

Lakini serikali ya Israel imesuta hoja hiyo. Waziri wa Israel Yuval Steinitz, anasema Israel daima imeunga mkono kuanza tena mazungumzo ya amani, lakini bila ya kuwepo masharti.

Pande zote zimekaribisha mkutano huo wa Jordan, wakisema wako tayari kubahatisha kupatikana amani . lakini tofauti kati yao bado ni kubwa na matarijio ya kupatikana suluhuisho ni ndogo.

XS
SM
MD
LG