Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 06:55

Jordan kukabiliwa na kipindi kigumu kutokana na migomo ya madereva wa malori


Mabasi yalioegeshwa kwenye mkoa wa Maan, Jordan, kutokana na mgomo wa madereva. Dec. 16, 2022
Mabasi yalioegeshwa kwenye mkoa wa Maan, Jordan, kutokana na mgomo wa madereva. Dec. 16, 2022

Wachambuzi wanasema kwamba Jordan huenda ikakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na wiki kadhaa za maandamano ya madereva wa malori, wanaolalamikia bei ya juu ya mafuta

Tatizo hilo limedumaza uchumi wa taifa, pamoja na kusababisha kifo cha afisa wa ngazi ya juu wa polisi. Polisi wengine watatu waliuwawa wakati wakiwasaka washukiwa wa mauaji ya afisa huyo, mmoja wao akishukiwa kuwa mwanamgambo wa kiislamu.

Serikali imefanya juhudi za kukutana na baadhi ya madereva hao, lakini kama anavyosema mchambuzi Osama al Sharif, kuna masuala mengi yanayohitaji kushughulikiwa, kabla ya hali ya kawaida kurejea. Amesema kwamba ongezeko kubwa la bei za mafuta limepelekea gharama ya juu ya maisha kwa wakazi wa Jordan.

Familia nyingi zinaripotiwa kutoweza kumudu bei ya mafuta ya kuweka joto wakati huu wa msimu wa baridi kali. Wakati huo huo ubalozi wa Marekani kwenye mji mkuu wa Amman umesema kwamba licha ya kupungua kwa maandamano, ni vyema raia wake wajiepushe kusafiri nje ya mji huo nyakati za usiku.

XS
SM
MD
LG