Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Agosti 20, 2022 Local time: 02:02

John Kerry aongoza juhudi mpya kuimarisha serikali ya Libya


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Italia Paolo Gentiloni, na mwakilishi wa Umoja wa mataifa Libya Martin Kobler katika mkutano huko Vienna, Austria, May 16, 2016.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry aliongoza juhudi mpya Jumatatu ili kuimarisha serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ili kuweza kupambana na ghasia zinazoendelea na uchumi unaodororra, lakini mkutano huo ulionekana haukuweza kupata ungaji mkono wa kutosha isipokua wajumbe kusema wa wataisaidia uongozi wa Libya unaokabiliwa na matatizo makubwa.

Kerry na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Boris Johnson waliitisha mkutano huo mjini London ambao ulijimuisha mawaziri kutoka Italia , Ufaransa, umoja wa falme za kiarabu na Saudia Arabia ambao walikutana na waziri mkuu wa Libya Fayez Saraj.

Mawaziri hao walithibitisha kile afisa wa wizara ya mambo ya nje alichosema ni uungaji mkono thabiti wa kimataifa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya, utawala wa mpito ambao hadi sasa haujafanikiwa kuchukua udhibiti wowote wa nchi hiyo isipokua mji mkuu wa Tripoli

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG