Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 10:44

John Dramani Mahama achukua madaraka Ghana.


Makamu rais wa Ghana John Mahama akiapishwa kuchukua madaraka.
Makamu rais wa Ghana John Mahama akiapishwa kuchukua madaraka.

Makamu rais wa Ghana John Dramani Mahama atamalizia muhula wa rais John Atta Mills .

Makamu rais wa Ghana John Dramani Mahama atamalizia muhula wa rais John Atta Mills ambaye alifariki ghafla Jumanne. Mahama aliapishwa kuchukua madaraka saa kadhaa baada ya maafisa kutangaza kifo cha Bw. Mills.

Ghana inatarajiwa kufanya uchaguzi ifikapo Desemba. Mchambuzi wa kisiasa Emmanuel Akwetey, mkurugenzi wa taasisi ya utawala wa kidemokrasia aliiambia VOA kwamba anatarajia chama tawala cha Democratic Congress kumtangaza Bw.Mahama kama mgombea wake. Alisema kwamba Bw.Mahama alifanya kampeni na hayati rais na kwamba muda uliobaki kabla ya upigaji kura ni mfupi.

Amesema chama cha upinzani cha New Patriotic Party kimesitisha kampeni zake kwa heshuima ya Bw. Mills na kusaidia kuunganisha nchi.

XS
SM
MD
LG