Jobs alikuwa na umri wa miaka 56 na alikuwa kisumbuliwa na saratani kwa takribani muongo mmoja.
Kampuni hiyo ya teknolojia imetoa taarifa kwenye tovuti yake Jumatano usiku, ikisema kampuni imempoteza mtaalamu makini na mwenye ubunifu na kwamba dunia imepoteza binadamu asiyeelezeka. Taarifa ya kampuni pia ilisema utashi wake utaendelea kuwa msingi wa milele wa Apple.
Rais wa Marekani Barack Obama alielezea rambirambi zake katika taarifa ya maandishi akisema Jobs alikuwa miongoni mwa wawekezaji wakubwa wa Marekani. Bwana Obama alisema Jobs aliunda kampuni nzima, alitengeneza mtandao sio tu kupatikana kiurahisi, lakini kitu makini na cha kuchangamsha na alifanikiwa kile alichokiita moja ya historia ambayo ni haba kupatikana ya kubadilisha namna tunavyoiona dunia.
Jobs alijiuzulu kama mkurugenzi mkuu wa kampuni ya technolojia mwezi Agosti. Alikuwa akiumwa saratani ya bandama tangu mwaka 2003 na alifanyiwa ubadilishaji wa ini mwaka 2009.
Katika taarifa ya maandishi, familia ya Jobs ilisema alikufa kwa amani Jumatano akizungukwa na wapendwa wake.