Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 15:10

Jeshi la Syria linaendelea kuua raia


mapambano kati ya waasi na jeshi la serikali nchini Syria katika jimbo la Latakia yasababisha vifo vya raia.

Kundi la kutetea haki nchini Syria linasema majeshi ya serikali yameua watu saba katika siku ya pili ya mapigano na waasi katika mkoa wa pwani ambo ulikuwa na utulivu. Hakuna wafuatiliaji wa Umoja wa Mataifa waliopelekwa katika mkoa huo.

Kundi hilo la Syrian Observatory for Human Rights lenye makao London limesema helikopta za kijeshi na vifaru vilishambulia miji kadhaa katika jimbo la kaskazini magharibi la Latakia siku ya Jumatano.

Mapigano kote nchini Syria siku ya Jumanne yameua zaidi ya watu 30, wengi wao ni wakazi wa Latakia, kundi la Observatory limesema. Habari za waliouawa hazikuweza kuthibitishwa na vyanzo huru.

Msemaji wa Umoja Mataifa mjini Damascus, Sausan Ghoshe ameiambia VOA kwamba tume ya ufuatiliaji ya Umoja wa Mataifa nchini Syria haina wafuatiliaji katika jimbo la Latakia. Amesema Umoja wa Mataifa imethibitisha kuhusu mapigano katika eneo hilo kwa kuongea na wawakilishi wa pande zote na haitapeleka wafuatiliaji wasiobeba silaha katika eneo ambalo ni hatari.

Lakini Ghosheh amesema mipango ya tume ni kuweka kituo katika mji wa pwani wa kaskazini magharibi wa Tartus ifikapo mwisho wa wiki na kupeleka doria huko Latakia haraka iwezekanavyo.

XS
SM
MD
LG