Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 03:35

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya kiislam Iran limeionya EU kuwaorodhesha ni magaidi


Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislam (IRGC) nchini Iran
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislam (IRGC) nchini Iran

Wabunge wa Bunge la Ulaya walipiga kura Jumatano kujumuisha IRGC kwenye orodha ya kigaidi ya mataifa 27 ya umoja huo kwa "kuzingatia shughuli zake za kigaidi, ukandamizaji wa waandamanaji na upelekaji  wake wa ndege zisizo na rubani kwa Russia"

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran siku ya Jumamosi liliuonya Umoja wa Ulaya dhidi ya kufanya "makosa" kwa kuliorodhesha kama kundi la kigaidi, baada ya bunge la umoja huo kutaka hatua hiyo ichukuliwe.

Wabunge wa Bunge la Ulaya walipiga kura Jumatano kujumuisha IRGC kwenye orodha ya kigaidi ya mataifa 27 ya umoja huo kwa "kuzingatia shughuli zake za kigaidi, ukandamizaji wa waandamanaji na upelekaji wake wa ndege zisizo na rubani kwa Russia".

Kura hiyo haina nguvu kisheria lakini inakuja huku mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wakiwa tayari wanatarajiwa kujadili kuimarisha vikwazo dhidi ya jamhuri hiyo ya Kiislamu wiki ijayo.

"Ikiwa wabunge hao wa ulaya watafanya makosa, lazima wakubali matokeo," mkuu wa IRGC Meja Jenerali Hossein Salami alisema, kulingana na tovuti ya Guards' Sepah News, katika matamshi yake ya kwanza juu ya hatua hiyo ya EU.

Umoja wa Ulaya "unafikiri kwamba kwa kauli kama hizi inaweza kulitikisa jeshi hili kubwa", Salami alisema.

"Hatuna wasiwasi kamwe kuhusu vitisho kama hivyo au hata kuvifanyia kazi, kwa sababu kadri maadui zetu wanavyotupa nafasi ya kuchukua hatua, tunafanya kwa nguvu zaidi," aliongeza.

Walinzi hao wanasimamia kikosi cha kujitolea cha Basij, ambacho kimepelekwa kuzuia maandamano tangu katikati ya mwezi Septemba yaliyosababishwa na kifo cha Mahsa Amini, mwenye umri wa miaka 22, baada ya kukamatwa kwake kwa madai ya kukiuka kanuni za mavazi za wanawake nchini Iran.

Mamlaka nchini Iran zinasema mamia ya watu, wakiwemo maafisa wa vikosi vya usalama wameuawa na maelfu kukamatwa katika ghasia hizo.

XS
SM
MD
LG