Haya ni kulingana na utawala wa Taliban ambao umeapa kulipiza kisasi dhidi ya jirani yao.
Naibu msemaji wa Taliban Hamdullah Fitrat amesema mashambulizi yametokea katika sehemu nne tofauti ndani ya Afghanistan. Amesema watu sita wamejeruhiwa.
Serikali ya Pakistan na maafisa wa jeshi hawajatoa taarifa kuhusu tukio hilo.
Afisa wa Pakistan mwenye taarifa kuhusu mashambulizi hayo, na ambaye hakutaka kutajwa na vyombo vya habari, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba Pakistan imetekeleza mashambulizi hayo dhidi ya kambi ya wapiganaji wa kiislamu wa Pakistan Taliban TTP.
Kundi la TTP lina ushirikiano na Taliban lakini halina uhusiano wa moja kwa moja na kundi la Talliban ambao sasa wanatawala Afghanistan. Lengo lake kubwa ni kuweka utawala unaofuata sheria za kiislamu nchini Pakistan, kama Taliban wanavyofanya nchini Afghanistan.
Forum