Makundi ya haki za binadamu nchini Misri yamelishutumu jeshi la nchi hiyo kwa kujaribu kulipiza kisasi dhidi ya makundi yanayounga mkono demokrasia kwa kushambulia ofisi zao.
Majeshi ya usalama ya Misri yalivamia ofisi 17 za haki za binadamu alhamisi kama sehemu ya uchunguzi ambao viongozi wa kijeshi wanasema utaonyesha jinsi fedha za nje zitakavyokuwa zimehusika kuchangia katika ghasia zinazoendelea.
Lakini taarifa iliyosainiwa Ijumaa na makundi 28 ya kiraia yanasema uvamizi huo ulikuwa ni sehemu ya kampeni kubwa ya kuwavunja nguvu wanaharakati ambao wanakosoa viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo.