Jeshi la Israel limetangaza leo Alhamisi kile ilichokiita “hatua mpya na zilizoboreshwa” za kuingiza misaada ya kibinadamu huko Ukanda wa Gaza, ikijumuisha kujenga kivuko kipya huko kaskazini mwa Gaza.
Msemaji wa jeshi Admirali Daniel Hagari amesema katika taarifa yake kwa njia ya video kwamba njia hiyo mpya ya kuvuka ardhi itawezesha misaada zaidi kuingia moja kwa moja kwa raia katika maeneo ambayo yamekuwa changamoto kwa malori hayo kufika.
Makundi ya kimataifa ya misaada ya kibinadamu yamelalamika kwa miezi kadhaa kuhusu vizuizi vinavyozuia kupeleka misaada kwa kutumia malori huko Gaza, yakitaja kuwa vizuizi vyote viwili vimecheleweshwa na jeshi la Israel na kutokuwa na njia salama ya kuyafikia maeneo kama vile kaskazini mwa Gaza kutokana na uharibifu wa vita.
Forum