Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 10, 2026 Local time: 17:28

Jeshi la Israel limefanya mashambulizi ya anga kuharibu mitambo ya makombora

Mashambulizi ya anga ya Israel yaliyolenga mitambo ya kurusha makombora. March 12, 2024.
Mashambulizi ya anga ya Israel yaliyolenga mitambo ya kurusha makombora. March 12, 2024.

Israel pia iliripoti Jumanne kufanya mashambulizi mapya ya anga katika eneo la Khan Younis kusini mwa Gaza

Jeshi la Israel limesema leo Jumanne kuwa lilifanya mashambulizi ya anga ili kuharibu mitambo mitatu ya kurusha makombora ambayo ilitumika kutuma sehemu ya roketi 100 zilizorushwa kutoka Lebanon kuelekea Golan Heights inayokaliwa na Israel.

Ghasia za mpakani ni duru ya hivi karibuni ya mapigano ya mara kwa mara ambayo yameongeza wasiwasi wa kimataifa kuhusu kuenea kwa vita vya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza hadi maeneo mengine katika eneo hilo.

Israel pia iliripoti Jumanne kufanya mashambulizi mapya ya anga katika eneo la Khan Younis kusini mwa Gaza wakati ikisonga mbele na kampeni yake ya kulitokomeza kundi la wanamgambo wa Hamas.

Wakati Umoja wa Mataifa umeonya juu ya kuongezeka kwa mzozo wa chakula huko Gaza, meli iliyokuwa na tani 200 za misaada iliondoka Cyprus leo ikiwa njiani kupeleka misaada kwa njia ya bahari.

This item is part of

Forum

XS
SM
MD
LG