Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 28, 2020 Local time: 21:13

Jeptoo arudia ushindi Boston marathon


wanaridha wa kimataifa wakiamba mbio za Maraton za Boston
Mwanadada Rita Jeptoo wa Kenya ameshinda mbio ndefu za Boston marathon kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya kuwatoka wapinzani wake kwa kasi kali katika kilomita tano za mwisho na kumaliza kwa rekodi mpya ya mbio za Boston.

Jeptoo ambaye alishinda mbio hizo mwaka jana alirudia ushindi wake katika muda wa saa 2 dakika 18 na sekunde 57, na hivyo kuvunja rekodi ya zamani ya Boston ambayo ilikuwa saa 2 dakika 20 na sekunde 43.

Mmarekani Meb Keflezighi, mzaliwa wa Eritrea, alishinda mbio za wanaume na kuwa mmarekani wa kwanza katika miaka kadha kushinda mbio hizo. Keflezighi alimaliza mbio hizo katika muda wa saa 2, dakika nane na sekunde 37, akimshinda Mkenya Wilson Chebet kwa sekunde 11 tu.

Mashindano haya yalikuwa ya kwanza mjini Boston tangu mashambulizi ya mabomu mwaka jana yaliyouwa watu watatu na kujeruhi mamia wengine. Mbio za mwaka huu zilikuwa na wakimbiaji 36,000 kulinganisha na 27,000 mwaka jana. Wakimbiaji kadha ambao walishindwa kumaliza mbio hizo mwaka jana kufuatia shambulio la bomu walikaribishwa kushiriki tena mwaka huu

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG