Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 22, 2025 Local time: 11:56

Jengo la ghorofa 5 limeanguka Syria na kuua watu 13


Eneo mahala ambapo jengo limeanguka katika mji wa Aleppo nchini Syria
Eneo mahala ambapo jengo limeanguka katika mji wa Aleppo nchini Syria

Wakati huo huo shirika la habari la Kikurdi na mfuatiliaji wa vita vya Syria limesema watoto watano ni miongoni mwa waliouawa na wote ni raia wa Syria waliokimbia makazi yao katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja wa mapigano nchini humo

Jengo lilianguka Jumapili katika mji wa pili kwa ukubwa wa Aleppo nchini Syria na kuua watu 13 wakiwemo watoto mamlaka na vyombo vya habari vimeripoti.

Shirika la habari la serikali SANA awali lilitoa idadi ya vifo 10 kabla ya kunukuu taarifa ya wizara ya mambo ya ndani inayoirekebisha idadi hiyo hadi 13 na kukadiria kuwa kuna uwezekano wa vifo kuongezeka.

Wakati huo huo shirika la habari la Kikurdi na mfuatiliaji wa vita vya Syria limesema watoto watano ni miongoni mwa waliouawa na wote ni raia wa Syria waliokimbia makazi yao katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja wa mapigano nchini humo.

Ni mtu mmoja tu aliyeokolewa kutoka kwenye kifusi wizara ya mambo ya ndani imesema ikiongeza kuwa juhudi za uokoaji na utafutaji zinaendelea.

Jengo hilo la ghorofa tano lilikuwa linakaliwa na familia saba, lilianguka nyakati za asubuhi siku hiyo wizara imeongezea.

Picha za video zilizosambazwa kwenye televisheni ya taifa ziliwaonyesha maelfu ya wafanyakazi wa uokozi wakiwa wakifukua watu kutoka kwenye vifusi huku malori makubwa yakifanya kazi ya kuondoa na kubeba vifusi hivyo.

SANA ilinukuu chanzo cha polisi kikisema awali kwamba jengo hilo, lililoko katika kitongoji cha Sheikh Maksoud mjini Aleppo lilianguka "kutokana na kuvuja maji" katika misingi ya jengo hilo.

Sehemu kubwa ya Aleppo iliharibiwa wakati wa mzozo wa Syria uliodumu kwa takriban miaka 12 huku majengo mengi yaliyobaki yakiachwa katika hali mbaya.

XS
SM
MD
LG